Kundi la Hezbollah la Lebanon limethibitisha kuwa kamanda wa kikosi katika eneo la kusini mwa Lebanon Ali Karaki na kiongozi mkuu wa kundi hilo Sayyed Hassan Nasrallah wameuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel yaliyolenga vitongoji vya kusini mwa mji mkuu Beirut.
Siku ya Ijumaa jioni, ndege za kivita za Israel zilishambulia makao makuu ya Hezbollah huko Dahieh, viunga vya kusini mwa Beirut, ambapo Nasrallah na baadhi ya makamanda wengine wa kundi hilo lenye silaha waliuawa.
Uvamizi huo uliharibu majengo kadhaa ya makazi, na kusababisha vifo vya watu 6 na wengine 91 kujeruhiwa.
Habari nyingine kutoka Wizara ya Afya ya Lebanon inasema watu wasiopungua 105 wameuawa na wengine 359 kujeruhiwa katika mashambulizi ya anga ya Israel nchini humo siku ya Jumapili.