Algeria na Niger zimejadili hatua muhimu za kujenga Bomba la Gesi linalopita kwenye jangwa la Sahara (TSGP) wakati wa ziara ya Waziri wa Petroli wa Niger Sahabi Oumarou nchini Algeria.
Nchi hizo mbili zimethibitisha utayari wao kwa ajili ya mradi huo, na Niger imeitisha mkutano wa ngazi ya juu wa mawaziri kutoka Algeria, Niger, na Nigeria kujadili hatua zinazofuata.
Bomba hilo la kilomita 4,000 linalounganisha Algeria, Nigeria, na Niger, litaunganishwa na mtandao uliopo wa bomba wa Algeria na kuwezesha usafirishaji wa gesi asilia kwenda Ulaya.
Mradi huo unakusudiwa kuimarisha usalama wa nishati, maendeleo ya kiuchumi ya kikanda, na kuimarisha ushirikiano wa nishati kati ya nchi hizo tatu.