Waziri Mkuu wa Ethiopia azindua kiwanda kikubwa zaidi cha saruji kilichojengwa na China nchini Ethiopia
2024-09-30 08:45:24| cri

Waziri Mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed amezindua Kiwanda cha Saruji cha Lemi kilichojengwa na China, kikiwa ni kikubwa zaidi cha saruji nchini Ethiopia chenye uwezo wa kuzalisha tani 15,000 kwa siku.

Akiongea kwenye uzinduzi wa kiwanda hicho, Bw. Abiy alisema mradi huo ni mfano wa utekelezaji wa haraka na wenye ufanisi wa ujenzi wa miundombinu muhimu.

Kiwanda hicho kilichojengwa kaskazini mwa mji wa Addis Ababa ambacho kinamilikiwa kwa ushirikiano kati ya kampuni ya China na ya Ethiopia, kina thamani ya dola za kimarekani milioni 600, na sasa kinazalisha asilimia 50 ya saruji nchini Ethiopia.