Serikali ya China yawatunuku wataalamu wageni tuzo ya Urafiki
2024-10-01 09:03:12| CRI

Serikali ya China imewatunuku wataalam 100 wageni Tuzo ya Urafiki ya Serikali ya China ya 2024 kwa kutambua mchango wao katika maendeleo ya China.

Mjumbe wa taifa wa China Bw. Shen Yiqin alitoa Tuzo ya Urafiki kwa waliopewa tuzo hiyo na kuahidi kuwa serikali itaweka mazingira mazuri zaidi kwa wataalam wa kigeni wanaoishi na kufanya kazi nchini China.

Bw. Shen pia amesema wataalam wageni wametoa mchango mkubwa katika harakati za kujenga usasa nchini China, jambo ambalo litakumbukwa na Wachina.