Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lin Jian amesema msaada wa kijeshi wa Marekani kwa mkoa wa Taiwan, bila kujali kiasi chake, hautayumbisha azma ya China ya kupinga ati " Uhuru wa Taiwan" na kulinda mamlaka ya taifa na ukamilifu wa ardhi ya China.
Msemaji huyo ameyasema hayo kufuatia taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Ikulu ya Marekani inayotangaza uamuzi wa Marekani wa kutoa msaada wa kijeshi kwa mkoa wa Taiwan wenye thamani ya karibu dola za kimarekani milioni 567.
Akijibu swali kwenye mkutano na wanahabari, Bw. Lin amesema kuupatia silaha mkoa wa Taiwan, Marekani kwa mara nyingine imekiuka kwa kiasi kikubwa kanuni ya China moja na taarifa tatu za China na Marekani, na hasa Taarifa ya Pamoja ya Agosti 17.