Mamlaka ya wanyamapori ya Kenya (KWS) imezindua mpango mkakati wa 2024 hadi 2028 ukionyesha njia ya kuimarisha ulinzi wa wanyamapori kote nchini Kenya.
Waziri wa Utalii na Wanyamapori Bibi Rebecca Miano, amesema mjini Nairobi kuwa lengo la mpango huo ni kuweka mkazo katika mbinu inayoongozwa na sayansi na inayoendeshwa na data katika usimamizi wa wanyamapori.
Amesema mpango huo unataka kuimarisha uchumi wa wanyamapori, kupunguza upotevu wa viumbe hai, kuboresha ushirikiano wa jamii, na kuleta manufaa kutokana na uhifadhi wa wanyamapori.
Bibi Miano ameongeza kuwa matarajio ya mpango huo ni kuifanya Kenya kuwa kwenye nafasi ya kuongoza kwenye utalii endelevu, na kutetea kuwa uchumi wa wanyamapori ni sawa na injini muhimu ya ukuaji.