Mkali wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz, anayefahamika kwa wimbo wake wa ‘Komasava’, anatazamiwa kushindana na wasanii wakubwa wa Nigeria katika tuzo zijazo za African Entertainment Awards USA (AEAUSA) mwezi Novemba.
Tangazo hili linafuatia kutangazwa kwa orodha ya walioteuliwa na AEAUSA, ambapo Diamond ameshirikishwa katika kitengo cha 'Msanii Bora wa Mwaka'.
Katika kipengele hiki, atakabiliana na ushindani mkali kutoka kwa wasanii nguli wa Afrika, akiwemo Burna Boy, Davido, Yemi Alade, Ayra Starr, Asake, Rema, Wizkid, Adekunle Gold, na nyota anayechipukia wa Afrika Kusini Tyla.
Mbali na kipengele cha 'Msanii Bora wa Mwaka', Diamond pia ametajwa kuwania 'Msanii Bora wa Kiume,' akichuana na wakali kama Davido, Burna Boy, Wizkid, Olamide, Rema, Kizz Daniel, Black Sherif, Fally Ipupa, na msanii aliyewahi kumsaini Harmonize.