Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema wahamiaji wasiopungua 45 wamefariki dunia baada ya boti mbili walizokuwa wakisafiria kuzama katika pwani ya Djibouti.
Shirika hilo limesema kupitia mtandao wa X, kuwa boti hizo ziliondoka Yemen zikiwa na watu 310, na hadi sasa ni watu 32 waliokolewa. Shirika hilo limesema kwa sasa linaisaidia serikali ya Djibouti kwenye utafutaji na uokoaji.