China yapinga Canada kuongeza kwa asilimia 100 ushuru wa ziada kwenye uagizaji wa magari ya umeme kutoka China
2024-10-02 10:24:56| cri

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Canada, nchi hiyo itaongeza kwa asilimia 100 ushuru wa ziada kwenye magari ya umeme yaliyotengenezwa nchini China kuanzia tarehe 1 Oktoba, pia imetangaza orodha ya bidhaa za chuma na alumini kutoka China ambazo zitaongezewa ushuru wa ziada kwa asilimia 25 kuanzia tarehe 2 Oktoba.

Wizara ya Mambo ya Nje ya China ikizungumzia suala hilo imesema hatua hizo za Canada zimekiuka kanuni za uchumi huria na ushindani wa haki, na kuharibu vibaya ushirikiano wa kawaida wa uchumi na biashara kati ya makampuni ya nchi hizo mbili, uhusiano wa uchumi na biashara kati ya pande hizo mbili, na kudhuru minyororo ya viwanda na usambazaji wa bidhaa duniani, na kwamba China itachukua hatua zote za lazima, ili kulinda kithabiti haki halali ya makampuni ya China.