Kenya yawataka wakimbizi na waomba hifadhi kukabidhi nyaraka za kusafiria
2024-10-02 09:39:57| cri

Kenya imewataka wakimbizi na watu wanaotafuta hifadhi kusalimisha pasipoti zao ndani ya siku 30 ili kulinda hadhi na haki yao chini ya sheria za kimataifa.

Kamishna anayeshughulikia maswala ya wakimbizi katika Wizara ya Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa wa Kenya Bw. John Burugu, amesema ameondoa kusitishwa kwa umiliki na utumiaji wa hati za kusafiria kutoka nchi za asili kwa mujibu wa sheria za kimataifa na sheria za Kenya, na kusema kushindwa kuzingatia agizo hili kunaweza kuwa na matokeo mabaya kisheria.

Amesema wakimbizi wanatakiwa kupata hati za kusafiria zinazoweza kusomeka kwa mashine, kupitia Idara ya Huduma za Wakimbizi kwa usafiri wowote nje ya Kenya.