Waziri wa Uganda asema uuzaji nje wa bidhaa kwa China kuongeza mapato ya fedha za kigeni
2024-10-02 10:02:37| cri

Waziri wa kilimo wa Uganda Bw. Frank Tumwebaze amewaambia waandishi wa habari kuwa makubaliano mawili yaliyosainiwa kati ya Uganda na China wakati wa mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwezi uliopita mjini Beijing, yameruhusu Uganda kuuza pilipili kavu na bidhaa za majini kwa China, ambayo yanatarajiwa kuongeza mapato ya fedha za kigeni ya Uganda.

Amesema bidhaa za aina hizo mbili za Uganda zitakumbatia soko kubwa la China baada ya kupitia ukaguzi husika wa mamlaka za nchi hizo mbili, na Uganda imejipanga vyema kukidhi mahitaji ya soko la China huku ikihakikisha ubora na usalama wa bidhaa zake.