Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia amefungua Kongamano la Kwanza la Kimataifa la uwekezaji wa Mnyororo wa Thamani wa Kilimo ili kusaidia kuhimiza sekta ya kilimo, ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Somalia.
Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji ya Somalia imeandaa kongamano la siku mbili kuhimiza ushirikiano, uwekezaji, na ukuaji endelevu wa sekta ya kilimo kwa nchi hiyo. Kongamano hilo limewaleta pamoja wawekezaji wa kimataifa, jumuiya ya wafanyabiashara, wafadhili na wataalam wa kilimo, ambao wanatafuta fursa endelevu za uwekezaji wa kilimo.
Kwenye hotuba yake ya ufunguzi, Rais Mohamud amesisitiza fursa zilizopo kwenye sekta ya kilimo nchini Somalia, akisema kuwa nchi hiyo iko katika nafasi ya kimkakati ya ukuaji na inapenda kufanya ushirikiano wa kimataifa utakaoleta ustawi.