Marais wa China na Russia wapongezana kwa kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili
2024-10-02 10:32:52| cri

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Russia Vladimir Putin leo wametumiana salamu za kupongeza miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili.

Kwenye salamu zake, Rais Xi amesema China na Russia ni majirani, na pia ni nchi kubwa duniani, na nchi muhimu zinazoibuka kiuchumi. Na katika miaka 75 iliyopita, nchi hizo mbili zimeendelea kuinua kiwango cha uhusiano wao, kufuatilia maslahi ya kimsingi ya nchi na wananchi. Amesisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na Russia kupanua ushirikiano wao halisi, kuhimiza maendeleo yenye sifa ya juu na ujenzi wa mambo ya kisasa, na kutoa mchango mpya kwa ajili ya kudumisha amani na utulivu duniani, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya yenye hatma ya pamoja ya binadamu.

Kwa upande wa Rais Putin, amesema hivi sasa kiwango cha uhusiano kati ya Russia na China kiko juu zaidi katika historia, nchi hizo mbili zimefanya ushirikiano katika nyanja mbalimbali zikiwemo siasa, uchumi na biashara, na sayansi na teknolojia, kuungana mkono katika mambo ya kimataifa na kikanda, na zinajitahidi kwa pamoja kujenga dunia yenye ncha kadhaa.