Israel yafanya mashambulizi kwa ndege katikati ya mji wa Beirut
2024-10-03 09:26:54| CRI

Israel imefanya mashambulizi kwa ndege dhidi ya kituo cha Mamlaka ya chakula chenye uhusiano na Hezbollah katika eneo la al-Bachoura, katikati mwa mji Beirut, na kusababisha moto mkubwa.

Picha za televisheni zimeonyesha moshi mzito mweusi ukifuka kutoka kwenye jengo hilo, na shambulizi hilo la anga pia limesababisha uharibifu mkubwa kwenye nyumba za jirani na magari yaliyoegeshwa.

Muda mfupi kabla ya shambulizi katikati mwa Beirut, Israel ilifanya mashambulizi mengine makubwa ya ndege kwenye eneo la Haret Hreik katika vitongoji vya kusini mwa Beirut, na kusababisha moto mkubwa. Jeshi la Israel limethibitisha kufanya mashambulizi hayo.