Zambia yaongeza usambazaji wa umeme hadi saa 3 huku kukiwa na shida ya nishati
2024-10-03 09:25:10| CRI

Watumiaji wa umeme nchini Zambia watapata umeme kwa saa tatu za umeme wa uhakika, wakati nchi hiyo inaendelea kukabiliana na tatizo la umeme lililosababishwa na ukame.

Akiongea na wanahabari kuhusu hali ya changamoto ya umeme nchini Zambia, Waziri wa Nishati Bw. Makozo Chikote amesema kutokana na kituo cha kuzalisha umeme cha Maamba kurejea katika uzalishaji kamili na kupitishwa kwa uagizaji wa umeme kutoka nje, usambazaji wa umeme ulio imara zaidi utaonekana nchini Zambia.

Bw. Chikote amesema tofauti na mwezi uliopita, wakati watumiaji walipokabiliwa na kukatika kwa umeme kwa muda mrefu bila kutabirika, hali hiyo inatarajiwa kuboreka kutokana na hatua ambazo serikali imetekeleza. Serikali imetatua changamoto za kiufundi zilizotatiza uagizaji wa umeme kutoka Namibia, na matengenezo katika kituo cha kuzalisha umeme cha megawati 300 cha Maamba yamekamilika.