Rais William Ruto wa Kenya amefungua maonyesho ya kimataifa ya utalii katika mji mkuu wa Nairobi, na kuthibitisha dhamira yake ya kuongeza idadi ya watalii kutoka masoko yanayoibuka.
Maonyesho ya Utalii ya Magical Kenya 2024, ambayo ni maonyesho ya utalii yanayoongoza katika eneo la Afrika Mashariki na Kati, yatafanyika hadi Ijumaa, na yamevutia zaidi ya washiriki 4,000 kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Maonyesho hayo ya siku tatu yaliyoandaliwa na Bodi ya Utalii ya Kenya(KTB), yanahudhuriwa na mawakala 180 wa usafiri wa kimataifa, wakiwemo 75 kutoka Afrika, 37 kutoka Amerika Kaskazini, 26 kutoka Ulaya, na 42 kutoka Asia na Mashariki ya Kati.