Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesisitiza umuhimu wa kudumisha sarafu thabiti ili kukuza utulivu wa uchumi wa Zimbabwe.
Akiongea kwenye hotuba aliyotoa kwenye jengo jipya la bunge za Zimbabwe, Rais Mnangagwa amesema utulivu wa sarafu ndio msingi wa uchumi mkuu, Kupitishwa kwa Dhahabu ya Zimbabwe (ZiG) Aprili mwaka huu, ilikuwa ni hatua muhimu ya kuleta utulivu wa sarafu ya ndani inayotegemezwa na akiba ya dhahabu na madini yenye thamani. Amesema ni jukumu la wazimbabwe wote kuheshimu na kutii hatua na mamlaka ili kudumisha utulivu wa kiuchumi na kudhibiti mfumuko wa bei.
Kauli ya Rais Mnangagwa imetolewa baada ya Benki Kuu ya Zimbabwe kupunguza thamani ya sarafu ya nchi hiyo kwa asilimia 42.6 dhidi ya dola ya Marekani, katika marekebisho yake ya kwanza ya kiwango cha ubadilishaji fedha tangu kuanza kutumika mwezi Aprili.