Shirika la Reli la Kenya (KRC) limetoa taarifa likisema huduma ya reli ya SGR iliyojengwa na China nchini Kenya, imeboreshwa baada ya kuongezwa kwa mabehewa mapya ya daraja la juu. Hatua hiyo inatarajiwa kuboresha huduma kwa abiria katika sekta mbalimbali ikiwemo ufanisi, anasa, usalama na urahisi.
Kwa mujibu wa KRC, nauli za mabehewa mapya zitabadilika kutegemea umri wa abiria.
Waziri wa Barabara na Uchukuzi wa Kenya Davis Chirchir amehudhuria sherehe ya uzinduzi wa huduma hiyo iliyoboreshwa.