Shirikisho la Soka la Cameroon lasikitishwa na hatua ya FIFA kumfungia rais wa Shirikisho hilo kutazama mechi za timu ya taifa kwa miezi sita
2024-10-03 15:07:31| CRI

Shirikisho la Soka la Cameroon (FECAFOOT) limeeleza kusikitishwa na hatua ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kumfungia Samuel Eto’o, rais wa FECAFOOT, kushiriki katika mechi za timu ya taifa hilo kwa kipindi cha miezi sita.

Jumatatu wiki hii, FIFA ilisema imemzuia mchezaji huyo wa zamani wa timu ya Barcelona baada ya kukutwa na hatia ya kukiuka kanuni za usawa katika mchezo na kuwatendea vibaya wachezaji na maofisa wakati wa michuano ya Kombe la Dunia la FIFA kwa Wanawake chini ya miaka 20, mzunguko wa 16 uliohusisha mechi kati ya Brazil na Cameroon, iliyochezwa mapema mwezi Septemba.