Mamlaka ya wanyamapori ya Kenya (KWS) imepongeza operesheni ya kuhamisha wanyamapori ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha maisha ya wanyamapori na kuimarisha uhifadhi wa makazi ya wanyamapori.
KWS imesema karibu tembo 50 watahamishwa kutoka mbuga ya taifa ya Mwea hadi Mbuga ya Aberdare katikati mwa Kenya. KWS imesema uhamishaji huo unaendana na mpango wa taifa wa usimamizi wa Tembo 2023-2032, ulioandaliwa na wakala na washirika wake, ambao unatoa wito wa kupata idadi endelevu ya tembo, kupunguza migongano kati ya binadamu na tembo, na kurejesha makazi yaliyoharibiwa.
Inatarajiwa kuwa hatua hii itapunguza shinikizo kwenye mbuga ya Mwea, ambako idadi ya tembo imeongezeka kutoka 49 ya mwaka 1979 hadi 156 ya sasa.