Idadi ya kesi zilizothibitishwa kuwa na ugonjwa wa Mpox nchini Uganda imeongezeka na kufikia 41 ndani ya wiki mbili.
Akizungumza kwenye Kongamano la Ushirikiano wa Nidhamu katika Utafiti wa Magonjwa kuhusu Mpox lililofanyika jumatano jioni nchini Uganda na kuhudhuriwa na wataalamu kutoka nchi za mashariki na katikati ya Afrika, naibu kamanda wa kushughulikia ugonjwa huo nchini Uganda, Atek Kagirita amesema, kwa sasa kuna wagonjwa 41 waliothibitishwa kuwa na ugonjwa huo, na wengine bado wametengwa na wanaendelea kufuatiliwa. Ameongeza kuwa, mpaka sasa hakuna vifo vilivyoripotiwa kutokana na ugonjwa huo na kwamba bado wanaendelea kufuatilia watu waliowasiliana kwa karibu na wagonjwa, ambao wengi wao ni jamii ya wavuvi.