Idadi ya waliokufa kwenye ajali ya kivuko nchini DRC yaongezeka na kufikia 87
2024-10-04 09:00:25| cri

Takriban watu 87 wamekufa kwenye ajali ya kuzama kwa kivuko kwenye Ziwa Kivu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Mamlaka za huko zimesema kivuko hicho kilichokuwa kinatoka katika mji wa Minova wa Kivu Kusini, kilipinduka karibu na bandari ya Kituku, nje kidogo ya mji wa Goma, wa Kivu Kaskazini.

Ripoti iliyotumwa kwa serikali kuu mjini Kinshasa, serikali ya mkoa pia imesema watu 78 bado hawajulikani walipo, na miili 87 ilipatikana.

Idadi kamili ya abiria waliokuwemo ndani ya boti hiyo bado haijajulikana, na imefahamika kuwa kivuko hicho kilikuwa kimejaza mzigo kupita kiasi. Kivuko hicho kilishindwa kustahimili wimbi kali kabla ya kupinduka takriban mita 700 kutoka bandarini.