Korea Kaskazini yasema itatumia nguvu zake zote pamoja na silaha za nyuklia kama itashambuliwa
2024-10-04 08:59:43| cri

Kiongozi mkuu wa Jamhuri ya Watu wa Kidemokrasia ya Korea (DPRK) amesema nchi hiyo itatumia nguvu zote ikiwa ni pamoja na silaha za nyuklia, kama maadui watajaribu kutumia vikosi vyenye silaha kuingilia uhuru nchi hiyo.

Kiongozi Mkuu wa nchi hiyo Kim Jong Un, amesema hayo alipokuwa akikagua kambi ya mafunzo ya kitengo maalum cha operesheni, na kusisitiza kuwa matamshi ya vitisho vya maadui, hila na majaribio havitaondoa silaha za nyuklia za nchi yake, na kwamba imepata nguvu kamili ya silaha za nyuklia na uwezo wa kuzitumia.

Kiongozi huyo pia amesema ni jambo la kijinga kuombea bahati kwenye mgogoro wa kijeshi na silaha za nyuklia, na kama mgogoro huo ukitokea uwepo wa Seoul na Jamhuri ya Korea hautawezekana.