Kura za maoni zaonyesha Rais wa Tunisia Kais Saied atashinda uchaguzi wa rais
2024-10-07 09:00:57| CRI

Habari kutoka Televisheni ya Taifa ya Tunisia zimesema kuwa kura za maoni zilizopigwa baada ya wapiga kura kutoka kwenye vituo vya kupigia kura zimeonyesha rais Kais Saied wa Tunisia anatarajiwa kushinda uchaguzi wa rais uliofanyika Jumapili.

Kwa mujibu wa makadirio ya matokeo ya kura ya maoni yaliyofanywa na Sigma Conseil, kampuni ya uchunguzi ya Tunisia, rais Saied amepata asilimia 89.2 ya kura, akifuatiwa na Ayachi Zammel aliyepata asilimia 6.9 na Zouhair Maghzaoui aliyepata asilimia 3.9.

Katika mkutano na wanahabari kufuatia uchaguzi huo, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi (ISIE) Farouk Bouaskar amesema wapiga kura waliojitokeza kwenye uchaguzi wa rais wamefikia asilimia 27.7. Na matokeo ya awali ya uchaguzi huo yatatangazwa Jumatatu jioni.