Bunge la Ethiopia lamteua waziri wa mambo ya nje kuwa rais mpya
2024-10-08 09:17:19| CRI

Mabunge mawili ya Ethiopia yamemteua Waziri wa Mambo ya Nje Taye Atske Selassie kuwa rais mpya.

Uteuzi huo ulifuatia kumalizika kwa muhula wa rais wa sasa Sahle-Work Zewde, baada ya kuongoza nchi kwa miaka sita.

Rais mpya aliyeteuliwa aliapishwa Jumatatu mbele ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Ethiopia na Baraza la Shirikisho na kuwa rais mpya wa nchi hiyo.

Akiwa na uzoefu wa kidiplomasia kwa muda wa miongo mitatu, ikiwa ni pamoja na jukumu lake kama mwakilishi wa kudumu wa Ethiopia kwenye Umoja wa Mataifa, Atske Selassie amekuwa waziri wa mambo ya nje kuanzia Februari mwaka huu hadi uteuzi wake mpya.