Walimu nchini Kenya watishia kususia usahihishaji wa mitihani
2024-10-08 18:50:23| cri

Muungano wa Walimu wa Sekondari nchini Kenya (KUPPET) umetishia kuwaongoza walimu kususia usahihishaji na usimamizi wa mitihani ya kitaifa kutokana na marupurupu duni.

Katibu Mkuu wa Muungano huo Akelo Misori, amesema wanachotaka ni malipo ya hadi Sh 4,000 kwa siku pamoja na malazi bora kwa walimu wanaosahihisha mitihani ya kitaifa.

Muungano huo umesema, kwa sasa, Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC) huwalipa watahini, waangalizi na wasimamizi wa vituo vya mitihani Sh 400, Sh 450 na Sh 500, kwa siku, lakini wasahihishaji wa mitihani hulipwa hadi Sh 150 kwa siku na kupewa makazi duni.

Bw Misori ameonya kuwa, endapo KNEC haitatoa jibu mwafaka, walimu watajitoa katika usimamizi na usahihishaji wa mitihani.