Wabunge nchini Kenya wapiga kura kumuondoa Makamu wa Rais madarakani
2024-10-09 10:59:11| cri

Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua ameondolewa madarakani licha ya kujitetea dhidi ya mashtaka ya ukiukaji katiba yaliyowasilishwa na Mbunge wa Kibwezi Magharibi, Mwengi Mutuse.

Jana jioni, wabunge 281 kati ya 349 walipiga kura ya ndio kumwondoa naibu huyo wa Rais madarakani, ikiwa ni miaka miwili tu tangu asaidie kuunda serikali ya Kenya Kwanza katika uchaguzi mkuu wa 2022.

Katika zoezi hilo, wabunge 44 walipiga kura ya hapana huku mbunge mmoja akikataa kupiga kura.

Gachagua amekua Naibu wa Rais wa kwanza katika historia ya Kenya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye, akidaiwa kuhusika na tuhuma mbalimbali, ikiwemo kujilimbikizia mali na uchochezi.