Africa CDC yatoa wito wa kutengeneza vifaa tiba kwa ajili ya maandalizi ya mlipuko wa maradhi
2024-10-10 10:39:52| CRI

Mkurugenzi wa Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) Jean Kaseya Jumatano alieleza wasiwasi wake juu ya Afrika kutegemea msaada wa nje kwenye vifaa tiba wakati wa kipindi cha mlipuko wa maradhi.

Akihutubia Kongamano la Biashara la Eneo la Biashara Huria Barani Afrika lililofanyika mjini Kigali nchini Rwanda, Kaseya alisisitiza kuwa Afrika inahitaji kujitegemea katika kutengeneza chanjo, dawa na uchunguzi wa ugonjwa.

Kaseya aliongeza kila linapotokea janga, Afrika inaingiwa na hofu, hali ambayo inalilazimisha bara hilo lianze kuomba chanjo, dawa na uchunguzi wa magonjwa kutoka nje. Alitoa wito wa kuchukua hatua mara moja kutengeneza vifaa tiba ndani ya Afrika.