Ripoti iliyotolewa na mwandishi maalum wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa Alena Douhan imesema, vikwazo vya upande mmoja vilivyowekwa na Marekani na washirika wake dhidi ya China vimekiuka sheria ya kimataifa, na China inakaribishwa kukabiliana na vikwazo hivyo kwa hatua za lazima ikiwemo ya kisheria.
Wakati huohuo, mamia ya nchi zimeeleza kuiunga mkono China kupitia njia mbalimbali, zikisisitiza kuwa masuala ya Xinjiang, Hong Kong na Tibet ni mambo ya ndani ya China, na zinapinga uingiliaji wa Marekani katika mambo hayo. Hali hii inaonesha kuwa vitendo vya nchi chache za Magharibi ikiwemo Marekani vya kulifanya suala la haki za binadamu liwe la kisiasa, havikubaliki kimataifa.