KESSHA yatoa tahadhari ya kufunga shule mapema kutokana na uhaba wa pesa
2024-10-10 23:18:47| cri

Shule za Upili nchini Kenya huenda zikalazimika kufungwa mapema baada ya serikali kushindwa kutoa pesa zinazohitajika kuendeleza shughuli kwa muhula wa tatu.

Shirikisho la Wakuu wa Shule za Upili nchini Kenya (KESSHA) limetoa tahadhari hiyo, likisema shule zinashindwa kununua bidhaa za kimsingi kwa maandalizi ya mtihani ujao wa kitaifa (KCSE) na mitihani ya kufunga mwaka kwa watahiniwa.

Kati ya Sh 22,244 kwa mwanafunzi zilizotarajiwa kutolewa chini ya mpango wa ufadhili wa elimu, serikali ilitoa Sh15,192 pekee, na kuagiza kiasi cha fedha hizo zitumike katika ujenzi wa miundombinu msingi.

Baadhi ya shule za Upili nchini Kenya tayari zimepanga kufunga shule Oktoba 18, 2024 ili kuepuka kukosa mahitaji ya kukidhi wanafunzi.