Mazishi rasmi yalifanyika Alhamisi huko Goma, mji mkuu wa Mkoa wa Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kuwakumbuka watu waliokufamaji kwenye ajali mbaya ya kivuko iliyotokea hivi karibuni kwenye Ziwa Kivu karibu na bandari ya Kituku.
Mazishi ya miili 11 iliyotambuliwa ya wakazi wa Goma waliofariki baada ya kivuko "MV MERDI" kuzama kwenye Ziwa Kivu wiki moja iliyopita yalifanyika katika makaburi ya Makao. Kwa mujibu wa ripoti ya serikali ya mkoa takriban watu 87 walifariki kwenye ajali hiyo, hata hivyo ripoti hiyo haikutaja idadi kamili ya watu waliokuwemo kwenye chombo.
Makamu Gavana wa jimbo hilo Jean Romuald Lipopo ambaye alikuwepo kwenye mazishi, alisema kivuko hicho kilivunjika vipande vitatu na kwa sasa kiko kwenye kina kirefu cha takriban mita 198 katika Ziwa Kivu, akibainisha kuwa gesi ya methane katika ziwa hilo imekwamisha juhudi za msako. Vyanzo vya ndani viliripoti kuwa kivuko hicho kilijaza kupita kiasi.