Watu mbalimbali kisiwani Taiwan wameonesha wasiwasi kutokana na matamshi ya hivi karibuni ya kiongozi wa Taiwan Lai Ching-te, kuhusu uhusiano wa pande mbili za mlangobahari wa Taiwan, wakimtuhumu kwa kurejesha nadharia yake mpya ya "nchi mbili" na kuichokoza China bara kwa makusudi.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa na chama cha Leba cha Taiwan na Baraza la Amani na Maendeleo la mlangobahari, inasema hotuba iliyotolewa na Bw. Lai siku wiki iliyopita, iligubikwa na upinzani kwa China bara na kukataa kuungana tena kwa taifa, kimsingi hotuba hiyo ni kurudisha msimamo wake wa kuitenga Taiwan kwa nadharia mpya ya "nchi mbili".
Kwenye hotuba aliyotoa Mei 20 wakati akiingia madarakani kama kiongozi wa mkoa wa Taiwan, Bw. Lai alitangza toleo jipya la nadharia ya "nchi mbili", akisisitiza kuwa pande mbili za Mlango wa Bahari sio za kila mmoja. Wachambuzi kisiwani Taiwan wana wasiwasi kwamba Bw. Lai tayari amewazidi watangulizi wake ikiwa ni pamoja na Lee Teng-hui, Chen Shui-bian na Tsai Ing-wen kwenye njia ya "uhuru wa Taiwan". Hotuba yake imekosolewa vikali na wadau mbalimbali wa Taiwan.