Rais wa China atoa salamu za pongezi kwa rais mpya wa Ethiopia
2024-10-14 08:39:54| cri



Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pongezi kwa Bw. Taye Atske-Selassie Amde kwa kuchaguliwa kuwa rais mpya wa Ethiopia.

Rais Xi amesema, uhusiano kati ya China na Ethiopia umepata maendeleo ya kasi kwa pande zote katika miaka ya hivi karibuni, uaminifu wa kisiasa kati ya nchi hizo mbili umeongezeka, na ushirikiano kati yao kwenye sekta mbalimbali umepata mafanikio makubwa. 

Rais Xi amesema anapenda kushirikiana na rais Taye kutumia fursa ya kutekeleza matokeo ya mkutano wa kilele wa mwaka 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, kuhimiza uhusiano wa kiwenzi na kimkakati kati ya China na Ethiopia, na kuwanufaisha wananchi wao.