Balozi wa China asema uhusiano wa China na Tanzania unaendelea kuzaa matunda
2024-10-14 13:52:21| cri

Balozi wa China nchini Tanzania, Bi. Chen Mingjian, amesema uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na China unaendelea kuchochea ushirikiano katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akiongea mkoani Njombe kwenye uzinduzi wa zahanati ya kibingwa, ambayo inayoendeshwa na serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na Ubalozi wa China, Balozi Chen amesema timu ya madaktari 27 bingwa kutoka China imeletwa ili kutoa huduma za kibingwa kwa Watanzania.

Akiongea kwenye uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Bw. Athony Mtaka, amesisitiza umuhimu wa wananchi kujenga utaratibu wa kuchunguza afya zao na kupata tiba, pamoja na uwepo wa madaktari bingwa na vifaa vya kisasa. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Bw. Juma Mfanga, ameongeza kuwa ubalozi wa China umeleta matibabu ya kibingwa ambayo yatatolewa bure.