Idadi ya vifo kutokana na mashambulizi ya anga ya Israel nchini Lebanon yafikia 2,306
2024-10-14 08:42:33| CRI

Wizara ya Afya ya Lebanon imesema, idadi ya vifo vilivyotokana na mashambulizi ya anga ya Israel nchini humo tangu Oktoba 8 mwaka 2023, imefikia 2,306, na wengine 10,698 wamejeruhiwa.

Kwa mujibu wa Wizara hiyo, Jumamosi iliyopita, watu 51 waliuawa na wengine 174 kujeruhiwa katika mashambulizi ya anga yaliyofanya na jeshi la Israel.

Tangu tarehe 23 mwezi Septemba, jeshi la Israel limekuwa likifanya mashambulizi makubwa ya anga nchini Lebanon kutokana na kuongezeka kwa mvutano na kundi la Hezbollah.