Kikosi cha muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL) kimetoa taarifa tarehe 13 mwezi huu kuwa alfajiri ya siku hiyo, vifaru viwili vya jeshi la Israel vimeharibu lango la kuingilia kituo cha kikosi hicho huko Ramyah na kuingia kwa nguvu. Licha ya hayo, UNIFIL pia imeshuhudia vikosi vitatu vya Israel vikivuka mstari wa Bluu na mlipuko wa makombora ulitokea karibu na kituo hicho na kusababisha walinda amani kumi na tano kuathiriwa kiafya.
Katika tarehe 10 na tarehe 11 mwezi huu, jeshi la Israel lilifanya mashambulizi dhidi ya UNIFIL na hadi tarehe 12, nchi 40 zimelaani kitendo hicho lakini imeonekana kudharauliwa kabisa na Israel. Wizara ya ulinzi ya Marekani imetoa taarifa ikisema waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin ameidhinisha kuweka mfumo wa THAAD wa ulinzi dhidi ya makombora nchini Israel pamoja na kutuma wanajeshi husika wa Marekani ili kuimarisha uwezo wa Israel wa ulinzi wa anga.