Tarehe 15 Aprili na 8 Julai mwaka huu, vituo vya Kichina vya Kukabiliana na Dharura ya Virusi vya Kompyuta pamoja na taasisi nyingine zilitoa ripoti mbili mfululizo, zikifichua nia halisi ya Marekani ya kuchafua sifa ya China kupitia mpango potoshi wa “Operesheni Volta Tyfoon”. Leo (tarehe 14), taasisi yetu ya usalama wa mtandao wa Internet imechapisha ripoti maalum mara ya tatu, ikifichua zaidi shughuli za ujasusi wa mtandao wa Internet na wizi wa siri uliofanywa na taasisi za serikali za Marekani na nchi washirika wa Jumuiya ya Five Eyes dhidi ya China, Ujerumani, na nchi nyingine, pamoja na ushahidi unaohusiana na jinsi taasisi za serikali za Marekani zinavyozituhumu nchi nyingine kwa njia mbalimbali. Aidha, ripoti hiyo inaonyesha ukweli wa mashambulizi ya “mlango wa nyuma”; yaliyofanywa na Marekani kwa kuingiza malengo yake katika vifaa vya mtandao internet, na hivyo hatimaye kufichua kwamba “Operesheni Volta Tyfoon”; ni drama ya kisiasa iliyoandaliwa na serikali ya shirikisho la Marekani yenyewe.
Ripoti inaonyesha kuwa kwa muda mrefu, Marekani imekuwa ikitangaza sera ya “ulinzi wa mapema” katika nafasi ya mtandao na kutekeleza operesheni ya “uwindaji wa mbele”, yaani, kupeleka vikosi vya vita ya mtandao katika maeneo ya nchi washindani na kufanya uchunguzi wa karibu na kupenya katika shabaha za mtandao wa internet katika nchi hizo.
Timu ya kiufundi imegundua kuwa Operesheni ya Volta Tyfoon ni operesheni ya taarifa potofu iliyotungwa na makundi ya kifedha ya Marekani kwa kuzingatia ushahidi uliokusanywa. Hii ni operesheni ya “Bendera Bandia” ya kawaida, ambayo njia na mbinu zake zinafanana kabisa na taasisi za kijasusi za Marekani na nchi washirika wa “Five Eyes”.
Uchunguzi wa timu ya kiufundi umegundua kuwa kwa mujibu wa nyaraka za siri za Idara ya Usalama ya Taifa ya Marekani, nchi hiyo ikitumia uwezo wake wa kiteknolojia na nafasi yake ya jiografia katika ujenzi wa mtandao, inadhibiti kabisa “vituo muhimu” vya mtandao kama vile nyaya za bahari za Atlantiki na Pasifiki, na imeanzisha vituo 7 vya taifa vya kusikiliza mawasiliano yote ya mtandao. Taasisi za serikali za Marekani na Kituo cha Usalama wa Mtandao cha Uingereza wanashirikiana kwa karibu katika kufafanua na kuiba data inayopitishwa katika nyaya hizo za bahari, na hivyo kufanikiwa kusikiliza watumiaji wa mtandao ulimwenguni bila kuchagua.