Wataalamu na maofisa watoa wito wa ushirikiano zaidi kati ya China na Afrika kupitia Pendekezo la Maendeleo ya Dunia
2024-10-14 08:45:27| CRI

Wataalamu na watunga sera kutoka mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na nchi za Afrika wamesisitiza haja ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa China na Afrika katika maeneo mbalimbali ya maendeleo endelevu.

Akizungumza katika mjadala uliofanyika hivi karibuni kuhusu Pendekezo la Maendeleo ya Dunia uliofanyika mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia, Kamishna wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi wa Umoja wa Afrika Mohamed Belhocine amesema, Pendekezo la China la Maendeleo ya Dunia lina uwezo wa kuimarisha zaidi uhusiano unaoendelea kukua wa China na Afrika na kupanua ushirikiano wa Kusini na Kusini.

Makamu mwenyekiti wa Mamlaka ya Kimataifa ya Maendeleo ya Ushirikiano ya nchini China, Zhao Fengtao amesema, China iko tayari kushirikiana na Afrika kutekeleza kikamilifu Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, na pia kuendelea kuimarisha maendeleo ya ushirikiano kati ya China na Afrika, na hatimaye kuchangia katika ujenzi wa jamii ya China na Afrika yenye hatma ya pamoja katika zama mpya.