Baraza la Usalama la UM lasema walinzi wa amani na maeneo ya UM hairuhusiwi kushambuliwa kamwe
2024-10-15 23:02:45| cri

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 14 Oktoba walitoa taarifa ya pamoja, wakieleza wasiwasi mkubwa kuhusu mapambano yanayoendelea kwenye mpaka wa “mstari wa bluu” kati ya Lebanon na Israel, ambayo yamesababisha kambi ya vikosi vya UM nchini Lebanon kushambuliwa na walinzi kadhaa wa amani kujeruhiwa, na kutoa wito kwa pande zote ziheshimu usalama wa walinzi wa amani na maeneo ya UM.

Mwenyekiti wa zamu wa Baraza la Usalama la UM kwa mwezi huu ambaye pia ni mwakilishi wa kudumu wa Uswisi kwenye UM Bibi Pascale Baeriswyl, ametangaza taarifa hiyo baada ya mkutano wa dharura kuhusu hali ya Lebanon. Amesisitiza kuwa walinzi wa amani na maeneo ya UM hairuhusiwi kushambuliwa kamwe.

Wajumbe wa Baraza la Usalama la UM wametoa wito kwa pande zote zifuate sheria ya kibinadamu ya kimataifa, na kutekeleza kikamilifu azimio namba 1701 la baraza hilo.