Rais Xi Jinping wa China jana amezungumza kwa simu na rais Joko Widodo wa Indoesia.
Katika mazungumzo hayo, rais Xi amesisitiza kuwa China iko tayari kushirikiana na Indonesia kukuza Kanuni Tano za Kuishi kwa Amani na Moyo wa Bandung, kuhimiza nchi za Dunia ya Kusini kushikamana, kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea, na kuhimiza kanda hiyo na dunia nzima kupata maendeleo, ustawi na utulivu.
Kwa upande wake rais Widodo ameishukuru China kwa mchango wake katika maendeleo ya kiuchumi ya Indonesia, na reli ya kasi ya Jakarta-Bandung imekuwa mfano mzuri kwa ushirikiano wa kujenga “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kati ya pande hizo mbili. Anaamini kuwa chini ya uongozi wa awamu mpya ya serikali ya Indonesia, uhusiano kati ya nchi hizo mbili utadumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo.