Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amezungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Israel, Bw. Israel Katz, ambapo Bw. Katz alielezea maoni ya Israel kuhusu hali ya kikanda.
Bw. Wang Yi amesema jumuiya ya kimataifa ina wasiwasi kuhusu kuzorota kwa hali ya migogoro katika eneo la Mashariki ya Kati na sasa mambo ya dharura yanayotakiwa kufanywa ni kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza, kuwaachia mateka na kuhakikisha misaada ya kibinadamu inafika katika ukanda huo bila vizuizi.
Pia ameeleza kuwa China inafuatilia sana hali ya mvutano kati ya Israel na Iran.
Amesema China siku zote haishiriki kwenye mambo ya ushindani ya kijiografia. Kwa kuwa China ni mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, inashikilia kuunga mkono amani, sheria ya kimataifa na hali halisi na itaendelea kuchangia kiujenzi katika juhudi za kutuliza mgogoro na kurejesha amani katika ukanda huo.