Uchumi wa Somalia unatarajiwa kuimarika hadi ukuaji wa asilimia 3.7 mwaka huu na asilimia 3.8 mwaka 2025.
Ripoti mpya ya benki ya maendeleo ya Afrika AfDB inasema ukuaji wa pato la taifa la Somalia utachochewa na ufufuaji wa mifugo ,huduma,fedha zinazotumwa kutoka nje na uwekezaji.
Eneo la kimkakati la nchi hiyo katika bahari ya shamu na bahari ya Hindi linaiweka kama kitovu cha usafirishaji cha kikanda kwenye ghuba.
Zaidi ya asilimia 80 ya mapato ya nje ya Somalia yanatokana na bidhaa za kilimo ambazo hazijasindikwa hivyo kuifanya nchi hiyo kukabiliwa na hali tete ya soko la bidhaa.