Kenya yathibitisha kifo cha kwanza kinachotokana na Mpox
2024-10-15 08:54:03| cri

Kenya jana imethibitisha kifo cha kwanza kinachotokana na ugonjwa wa mpox, huku kesi za ugonjwa huo zikiendelea kuongezeka nchini humo.

Katibu mkuu wa Wizara ya Afya ya Kenya Bi. Mary Muthoni, amesema kuwa idadi ya kesi zilizothibitishwa za ugonjwa wa mpox nchini humo sasa zimefikia 13. 

Bi. Muthoni amesema wagonjwa wanane kati ya hao wamepona kabisa, na wengine wanne wanaendelea kupata matibabu katika hospitali tofauti. 

Amesema mgonjwa aliyefariki alikuwa na matatizo mengine ya kiafya.