Tantrade Tanzania kuwania tuzo za kibiashara WTPO
2024-10-15 23:19:32| cri

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) imeorodheshwa kuwania Tuzo za Shirika la Kukuza Biashara Duniani (WTPO) mwaka 2024 kati ya mashirika manane ya kitaifa ya kukuza biashara yaliyoteuliwa kuwania tuzo hiyo mwaka huu na Kituo cha Biashara cha Kimataifa (ITC).

Tuzo za WTPO 2024 zinaangazia utendaji kazi bora wa mashirika ya kutangaza biashara (TPO) kwa kuainisha mipango ya maendeleo ya uuzaji bidhaa nje. Mipango ya maendeleo ya mauzo ya nje yanalenga kujenga uwezo wa biashara zinazouza nje katika muda wa kati na mrefu.

Tantrade ni miongoni mwa mashirika matatu yaliyoteuliwa kushindania kipengele cha 'Matumizi Bora ya Teknolojia ya Habari' kwa mpango wake wa kuanzisha tovuti ya biashara Tanzania iliyozinduliwa Julai 8, 2021, ili kutoa mwongozo wa kina na wa wazi kwa wafanyabiashara wanaoshughulika na biashara ya nje, uagizaji na usafirishaji.

Toviti hiyo inalenga kurahisisha mchakato wa biashara kwa kupunguza muda unaopotea na gharama katika kupata vibali na leseni.

Mashirika mengine ya kukuza biashara yaliyoteuliwa katika kipengele hicho ni pamoja na Jamhuri ya Dominika na Uswizi.

Kwa kuteuliwa katika mojawapo ya vipengele vya Tuzo za WTPO, Tantrade inatambulika kwa uwezo wake wa kuimarisha ushindani wa kibiashara wa Tanzania duniani kote.