Mamlaka ya Usimamizi wa Volkano huko Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imesema, volcano katika Mlima Nyamulagira imelipuka kuanzia Jumamosi iliyopita na mpaka jana jioni ilikuwa bado inaendelea kulipuka.
Mkurugenzi wa kisayansi katika Mamlaka hiyo Charles Balagizi amesema, moto mkali unaonekana katika kilele cha volcano ya Nyamulagira kutokea katika mji wa Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini.
Volcano ya Nyamulagira inafahamika kama moja ya volcano hai zaidi barani Afrika, na iko katikati ya Hifadhi ya Taifa ya Virunga, ambayo eneo lake kubwa linakaliwa na waasi wa kundi la M23, na hivyo kuathiri juhudi za Mamlaka ya Usimamizi wa Volkano kufuatilia mlipuko huo.