Benki Kuu ya Tanzania yakadiria ukuaji wa uchumi kuwa asilimia 5.6 katika robo ya tatu ya mwaka huu
2024-10-15 13:03:34| cri

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imekadiria kuwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania katika robo ya tatu ya mwaka huu, kuwa ni asilimia 5.6, na inatarajiwa kuwa katika robo ya nne ya mwaka kutakuwa na ukuaji wa asilimia 5.8, ukichangiwa na ongezeko la uwekezaji katika sekta ya umma na sekta binafsi.

Kwenye ripoti yake ya sera ya fedha iliyotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita, benki hiyo imesema ukuaji unaotarajiwa unaimarishwa na maboresho katika hali ya uchumi wa ndani na wa kimataifa. Wachangiaji wakubwa wa ongezeko hilo wametajwa kuwa kwenye sekta za ujenzi, kilimo, utalii, shughuli za kifedha na bima, viwanda, biashara na ukarabati, usafirishaji na uhifadhi wa shehena.

Ripoti pia imesema ukuaji huo utaimarishwa kwa kuboresha shughuli za kilimo kutokana na upatikanaji wa pembejeo za kilimo.