Volkano ya Nyamulagira nchini Jamhuri ya Kidemokraisa ya Kongo yalipuka
2024-10-16 11:06:48| cri

Volkano ya Nyamulagira iliyoko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imekuwa ikilipuka tangu Oktoba 12, huku uji wa moto ukitoka kwenye mdogo wa volcano hiyo na kumiminika kaskazini, magharibi na kusini magharibi mwa mlima.

Mkurugenzi wa Idara ya ufuatiliaji wa Volkano ya Goma Bw. Charles Balagizi amesema volkano hiyo inatokea kwenye milima ya Virunga kilomita 25 kaskazini mwa Ziwa Kivu.

Picha za hivi karibuni za satelaiti zimeonesha kuwa mtiririko wa uji wa volkano kwenye maeneo matatu, na mtiririko mrefu zaidi umesafiri karibu kilomita 7.