Ushirikiano kati ya Angola na China wachochea maendeleo ya pamoja
2024-10-16 08:40:41| CRI

Katibu wa idara ya sera na maendeleo ya makada iliyo chini ya chama tawala cha Angola MPLA, Angela Braganca amesema, ushirikiano wa muda mrefu kati ya Angola na China umeimarisha urafiki kati ya nchi hizo, na kuchochea maendeleo na ustawi wa pamoja.

Akizungumza katika hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa 6 wa Mwaka kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu ya China, Bi. Braganca amesisitiza umuhimu wa mabadilishano ya kitamaduni na kielimu kati ya China na Angola. Amesema moja ya ajenda muhimu ya mkutano huo inayohusu uzoefu wa China katika kuondokana na umasikini, ina umuhimu mkubwa kwa uongozi wa Angola.

Mkutano huo ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Renmin cha China, unatarajiwa kumalizika hii leo kwa majadiliano kati ya wasomi na wawakilishi kutoka China na wajumbe wa MPLA na wasomi wa Angola kuhusu njia za kuondokana na umasikini, ushirikiano kati ya China na Afrika, na utandawazi wa kiuchumi.