China yafuatilia maendeleo ya hali ya Peninsula ya Korea
2024-10-16 08:39:47| CRI

Vyombo vya habari vya Korea Kusini vimeripoti kuwa, Korea Kakazini imelipua sehemu ya barabara kwenye mpaka kati ya nchi hiyo na Korea Kusini.

Akizungumzia suala hilo, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Mao Ning amesema, China ikiwa nchi jirani ya Peninsula ya Korea, inafuatilia maendeleo ya hali ya Peninsula hiyo na mwelekeo wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Pia amesema hali ya wasiwasi ya Peninsula hiyo haiendani na maslahi ya pamoja ya pande zote, na kwamba kazi kuu kwa sasa ni kuepuka kuongezeka zaidi kwa mvutano. Pia amesisitiza kuwa China siku zote inaunga mkono kulinda amani na utulivu wa Peninsula ya Korea, msimamo wake wa kuhimiza ufumbuzi wa kisiasa wa suala la Peninsula hiyo haubadiliki, na inatumaini kuwa pande zote zitafanya juhudi za pamoja kufikia lengo hilo.