Rais Xi Jinping wa China Oktoba 15 alifanya ziara ya ukaguzi mjini Zhangzhou mkoani Fujian, ambapo alitembelea kjiji cha Aojiao wilayani Chenzhen, jumba la kumbukumbu la Gu Wenchang na bustani ya utamaduni ya Guandi na kufahamu hali ya kukuza ustawi wa vijiji, kuenzi moyo wa kimapinduzi na kuimarisha uhifadhi wa urithi wa kiutamaduni.